Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 13Article 551449

Habari Kuu of Friday, 13 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Bilioni 300 zimeidhinishwa kuijenga Dodoma

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa, Samia Suluhu Hassan ameidhinisha shilingi bilioni 300 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa makao makuu ya nchi jijini Dodoma.

"ndugu watanzania kama mnavyoona ujenzi wa Makao Makuu ukiendelea, ni pamoja na mji wa kiserikali, Rais samia ameshatoa bilioni 300, kwa ajili ya majengo ya Wizara ya kudumu na katika hizo bilioni 131 zitatumika kujenga Makao Makuu za ofisi za Wizara zote 23, na zote zitakuwa na ghorofa kuanzia 5 na kuendelea, kazi hiyo itaanza kuanzia mwezi septemba"

Aliwataka wahusika wote kuanza mara moja mchakato wa ujenzi huo, na kuwataka wasiwasahau Suma JKT kuwa mmoja wa watakao shiriki ujenzi wa majengo hayo kwani wanakidhi vigezo vyote.