Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 26Article 539992

xxxxxxxxxxx of Wednesday, 26 May 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Bilioni  323.39/- kumaliza adha ya umeme mikoa ya magharibi

HATIMAYE wananchi wa mikoa ya magharibi hususani Mkoa wa Kigoma wataondokana na adha ya umeme unaozalishwa kwa majenerata baada ya Serikali ya Tanzania kusaini mikataba miwili yenye thamani ya Sh bilioni 323.39 na Benki ya Maendelo ya Afrika (AfDB) kwa ajili ya mradi wa kufua umeme wa Malagarasi.

Kwa upande wa Tanzania, mikataba hiyo ilisainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Tutuba na Mkurugenzi Mkuu wa Kanda ya Afrika Mashariki wa AfDB, Nnenna Nwabufo.

Tukio hilo limefayika leo Dar es Salaam ambapo mara baada ya kusaini, Tutuba alisema mradi huo utachukua muda wa miaka mitano na utagharimu jumla ya Dola za Marekani milioni 144.1 ambapo Dola milioni 120 zitatolewa na AfDB, Dola milioni 20 zitatolewa na Africa Growing Together Fund na Dola milioni 4.14 zitatolea na Serikali ya Tanzania.

Kwa upande wake Nwabufo alisema mradi huo utawawezesha wananchi kupata umeme wa uhakika kwa gharama nafuu.

Join our Newsletter