Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 23Article 543979

Habari za Mikoani of Wednesday, 23 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Bilioni 66.8/- kuvifikishia umeme vijiji 233

Bilioni 66.8/- kuvifikishia umeme vijiji 233 Bilioni 66.8/- kuvifikishia umeme vijiji 233

VIJIJI 233 katika Mkoa wa Morogoro vitafikiwa na umeme kupitia mradi unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) baada ya Serikali kutenga zaidi ya Sh bilioni 66.8 ili kumalizia mradi huo awamu ya tatu ya mzunguko wa pili.

Waziri wa Nishati, Dk Merdad Kalemani amesema hayo katika uzinduzi wa mradi wa usambaza umeme vijijni ulifanyika katika Kijiji cha Muhezaititu katika Kata ya Rubeho wilayani Gairo mkoani humo.

Amesema mkoa huo una vijijini 673. Kati ya hivyo, vilivyowekwa umeme ni 440.

Katika awamu hiyo, Serikali itakamilisha vijiji vyote vilivyosalia.

Kalemani amesema gharama za kuweka umeme ni Sh 27,000, hivyo mwananchi yeyote atakayetozwa gharama zaidi, anapaswa kutoa taarifa katika vyombo vya ulinzi na usalama ili hatua za kisheria zichukuliwe.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Martine Shigella, amesema mradi huo wa usambazaji umeme vijijini utasaidia kuongeza uzalishaji wa viwanda kutokana na mkoa huo kulima mazao mbalimbali.

Amesema wananchi mkoani Morogoro wanalima mazao mengi yakiwemo ya mpunga, mahindi na alizeti, hivyo kutasaidia kuongeza kipato kwa mtu mmoja mmoja kwa kuongeza fursa za ajira.

Mkazi wa kijiji hicho, Amina Lumambo, amesema kitendo cha kufikishwa umeme katika eneo hilo ni jambo hawakutegemea kuwa litatokea.

Amesema kijiji hicho kinajihusisha na ufugaji wa mifugo mbalimbali ambao kwa sasa wameazisha kiwanda cha kutengeneza viatu na mikanda kwa kutumia ngozi, lakini wanashindwa kufanya kazi usiku kutokana na kukosa umeme.