Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 07Article 583990

Habari za Mikoani of Friday, 7 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Bilioni 7.6 kupeleka maji vijiji 47 Manyara

Bilioni 7.6 kupeleka maji vijiji 47 Manyara Bilioni 7.6 kupeleka maji vijiji 47 Manyara

Wananchi wa vijiji 47 wa Mkoa wa Manyara watanufaika na miradi ya maji baada ya wakala wa maji na usafi wa mazingira (Ruwasa) kusaini mikataba 12 yenye thamani ya Sh7.6 bilioni.   Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere akizungumza mjini Babati leo Ijumaa Januari 7, 2022 wakati wa kusainiwa kwa mikataba hiyo 12 amewataka walioshinda zabuni hizo kufanikisha miradi hiyo kwa wakati.

Makongoro amesema miradi hiyo ya maji ikikamilika wananchi 88,608 sawa na asilimia 4.9 ya wakazi wa Manyara, watanufaika na huduma ya maji.

Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Manyara, Mhandisi Walter Kirita ametaja baadhi ya maeneo yatakayonufaika na miradi hiyo ni Mbulu miradi saba, Babati miradi minne, Hanang' mmoja, Kiteto mmoja na Simanjiro mitatu.

Mbunge wa Jimbo la Simanjiro, Christopher Ole Sendeka amesema katika mkoa wa Manyara, wilaya za Simanjiro na Kiteto ndizo zina changamoto kubwa ya ukosefu wa maji.

Mmoja kati ya walioshinda zabuni hiyo, mwakilishi wa kampuni PNR Services Ltd, Frank Kitega amesema wanatarajia kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.

Advertisement