Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 13Article 585547

Habari Kuu of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Billion 2.3 zatendewa Haki Rorya kwa Kujenga Madarasa 113 na Ofisi 44

Billion 2.3 zatendewa Haki Rorya kwa Kujenga Madarasa 113 na Ofisi 44 Billion 2.3 zatendewa Haki Rorya kwa Kujenga Madarasa 113 na Ofisi 44

Wilaya ya Rorya ilipokea Shilingi Bilioni 2.3 kutokana na fedha za mkopo nafuu aliochukua Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Yetu Samia Suluhu Hassan kwenye Mradi wa Maendeleo kwa ustawi na Mapambano ya Uviko 19 kwa ajili ya Ujenzi wa Madarasa 113 na bweni 1.

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe Ally Salum Hapi amekabidhiwa vyumba vya Madarasa 113, Sekondary 98 na Shikizi 15 vilivyoambatana na ofisi 44 ambazo Wilaya imejenga ofisi hizi kwa kujiongeza.

Katika ziara yake hiyo alitembelea Miradi ya Maendeleo Sekta za elimu na afya alitembelea na kukagua Ujenzi wa Kituo Cha afya Cha Nyamagalo kilichopewa million 250 za fedha za Tozo.

Kupitia mradi huu Rorya tumetoa ajira za muda mfupi 1,234 kwa mafundi wa majengo, Mafundi wa Viti meza na madawati, Mafundi Umeme na mama lishe na huduma zingine.

Kipekee tunamshukuru Sana Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano Mama Samia kwa kuendelea kufungua milango Mbalimbali ya Maendeleo Wilaya ya Rorya.