Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 29Article 544645

Habari za Afya of Tuesday, 29 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Bima ya afya kutumia alama ya vidole badala ya kadi

Bima ya afya kutumia alama ya vidole badala ya kadi Bima ya afya kutumia alama ya vidole badala ya kadi

MFUKO wa Bima ya Afya umesema kuanzia Julai 11, mwaka huu utaanza kutumia alama za vidole kwa wanachama wake kupata matibabu na haitaruhusu hospitali na vituo vya afya kupokea kadi.

Mfuko huo unatarajia kuandikisha wanachama na wategemezi wao ambao hawajasajiliwa kwenye mfumo wake wa kielektroniki wa usajili kabla ya kuanza kutumika.

Mfuko huo unahudumia wananchi takribani milioni 25 na kati yao milioni saba ni wanachama wao.

"Wanachama na wategemezi wao wanaweza kutembelea vituo vya huduma vya NHIF vya karibu au hospitali nchini kote kujiandikishwa," alisema Mkurugenzi Mtendaji wa mfuko huo, Peter Kamunyo.

Awali, wanachama walitumia kadi za NHIF kupata huduma na mfumo uliokumbwa na ulaghai na sasa utatumika wa kielektroniki ili kuwatambua wanachama na wategemezi wao kwa alama za vidole.

Usajili wa alama za vidole umefanywa katika kaunti za Laikipia, Nakuru, Homa Bay, Kisumu, Tharaka Nithi, Taita Taveta na Nyeri.

Kamunyo alisema kwa mwezi wanahudumia wagonjwa takribani milioni moja, kati yao wanaolazwa 200,000 na wanaotibiwa na kuondoka wakiwa takribani 600,000 mpaka 700,000.

Katika mwaka wa fedha wa 2019/2020, mfuko huo ulikusanya Sh bilioni 60.81 kutoka kwa wanachama wake na ulilipa madai ya Sh bilioni 54.3.