Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 25Article 573949

Habari Kuu of Thursday, 25 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Bodaboda Kutengewa Eneo Maalum Barabarani

Bodaboda Kutengewa Eneo Maalum Barabarani Bodaboda Kutengewa Eneo Maalum Barabarani

JESHI la Polisi kwa kushirikiana na wadau wa usalama barabarani limezindua alama na maeneo maalumu ambayo yatasaidia kudhibiti ajali barabarani. Maeneo hayo yatafahamika kama 'buffer zone.'

Akizindua mpango huo katika eneo la Sanawari jijini Arusha, Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amepongeza hatua hiyo na kutaka isambazwe kwenye miji na mikoa mingine.

Buffer zone ni eneo la kudhibiti ajali ambapo kwenye alama za barabarani imeongezeka michoro mipya yenye alama ya bodaboda kabla ya kuvuka taa za kuongoza magari.

Michoro hiyo iliyochorwa chini ndio eneo ambalo bodaboda watasimama wakati wa kusubiri taa za barabarani ili kuepusha mgongano na magari yatakayokuwa yamesimama nyuma yao.

Aidha Waziri Simbachawene amewataka madereva kuzingatia sheria za barabarani katika maeneo hayo ili kuepusha ajali.