Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 06Article 541270

xxxxxxxxxxx of Sunday, 6 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Bodi zaagizwa kuelimisha utunzaji vyanzo vya Maji

WAZIRI wa Maji, Juma Aweso (pichani) ametoa maelekezo kwa Bodi za Mabonde yote nchini kuelimisha wananchi juu ya utunzaji wa vyanzo vya Maji.

Aidha, amezitaka Mamlaka za Maji kuhimiza

wananchi kutumia maji kwa uangalifu kulipia ankara za maji na kulinda miundombinu ya maji.

Waziri aweso alisema hayo jana mara baada ya kumalizika kwa upandaji miti ya matunda katika Ofisi za Wizara ya Maji zilizopo Mji wa Serikali Mtumba jijini hapa ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya

Mazingira Duniani ambayo kilele chake kitakuwa leo.

“Suala la mazingira ni suala nyeti sana, ukihifadhi mazingira yatakulinda na usipotunza mazingira athari zake huwa ni kubwa ni lazima tutunze vyanzo vya maji kwa kuweka mazingira vizuri lakini pia naipongeza Menejimenti ya Wizara kwa kusimamia vyema utun-zaji wa miti iliyopandwa katika aneo hii ni matumaini yangu kuwa miti hii iliyopandwa leo utasimamiwa

vizuri,suala la mazingira ni suala nyeti sana ukiifadhi mazingira yatakulinda” alisema Aweso.

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo, Nadhifa Kemikimba alisema miti ikipandwa husaidia kuwa na mazingira bora, kuwa na maji ya kutosha lakini na kusaidia kufanikisha malengo ya kupata maji safi na salama: “Huwezi kuwa na maji safi kama hujatunza Mazingira” alisema Kemikimba.

Maadhimisho ya siku ya Mazingira hapa nchini yanaratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira na kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Tumia Nishati Mbadala, Kuongoa mfumo Ikolojia’.

Join our Newsletter