Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 21Article 552883

Siasa of Saturday, 21 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Bosi wa zamani ATCL alipa faini akwepa kifungo

Bosi wa zamani ATCL alipa faini akwepa kifungo Bosi wa zamani ATCL alipa faini akwepa kifungo

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mataka

kulipa faini ya Sh milioni nane au kwenda jela miaka minne baada ya kupatikana na hatia katika mashitaka sita likiwamo la kuisababishia serikali hasara ya zaidi Sh bilioni 71.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo, ni aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Dk Ramadhan Mlinga na aliyekuwa Mwanasheria wa mamlaka hiyo, Bertha Soka ambao walihukumiwa faini ya Sh milioni mbili kila mmoja au kifungo cha mwaka mmoja gerezani.

Akisoma hukumu, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Janet Mtega alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi 18 wa upande wa mashitaka bila kuacha shaka kuwa washtakiwa wametenda makosa yao.

Katika hukumu hiyo ambayo washitakiwa wote

walilipa faini na kuachiwa huru, Mtega alisema mahakama imemuachia Mataka katika mashitaka ya kuisababishia serikali hasara ya Dola za Marekani 42,459,316.12 kwa sababu upande wa mashitaka ulishindwa kuthibitisha mashitaka hayo.