Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 20Article 552763

Uhalifu & Adhabu of Friday, 20 August 2021

Chanzo: MWANANCHI

Bosi wa zamani ATCL kulipa faini Tsh. Milioni 8 au jela miaka 8

Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL , David Mattaka Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL , David Mattaka

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka kulipa faini ya Sh8 milioni au kutumikia kifungo cha miaka minne jela baada ya kupatikana na hati ya makosa manne yaliyokuwa yakimkabili.

Mattaka amekutwa na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka, matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia hasara Serikali ya Sh71 bilioni.

Mbali na Mataka, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu mstaafu, Dk Ramadhan Mlinga na aliyekuwa Mwanasheria wa PPRA , Bertha Soka, ambao wamehukumiwa kulipa faini ya Sh2 milioni kila moja au kwenda jela mwaka mmoja ,baada ya kupatikana na hatia ya katika shtaka moja la kughushi mhutasari wa kikao.

Uamuzi huo umetolewa leo, Agosti 20, 2021 na Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili hukumu