Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 04Article 541060

Habari Kuu of Friday, 4 June 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Breaking: Ole Sabaya Afikishwa Mahakamani - Video

Breaking: Ole Sabaya Afikishwa Mahakamani - Video play videoBreaking: Ole Sabaya Afikishwa Mahakamani - Video

Breaking: Ole Sabaya Afikishwa Mahakamani – Video June 4, 2021 by Global PublishersAliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha akiwa na wenzake watatu leo Ijumaa, Juni 4, 2021, ili kusomewa mashitaka yanayomkabili. Sabaya alisimamishwa kazi na Rais Samia Suluhu kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.Sabaya amefikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa polisi akiwa na walinzi wake sita na baada ya kushuka kwenye magari pamoja na wenzake walitakiwa kuchuchumaa kusubiri taratibu nyingine.Baada ya muda mfupi walichukuliwa na kupelekwa katika chumba maalum wakisubiri kupelekwa mahakamani.Kwa takribani wiki moja Sabaya alikuwa akihojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) kwa tuhuma mbalimbali jijini Dar es Salaam. 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)Join our Newsletter