Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 06Article 555667

Siasa of Monday, 6 September 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

CCM Yatoa Maagizo kwa Serikali Sakata la Bei ya Mahindi

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo. play videoKatibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeiagiza Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), kununua tani 100,000 za mahindi ya wakulima katika Mikoa ya Nyanda za juu Kusini kikidai kuwa kimebaini wakulima wanapata shida ya soko la zao hilo.

Akizungumzia sakata hilo, Katibu Mkuu wa CCM amesema, “Hatuwezi kukaa namna hii wakulima wetu hawana pa kuuza mahindi yao, hivyo maagizo ya chama kwa serikali, watafute fedha popote wanapojua na suala la kununua mahindi liendelee kwenye maeneo yote ya uzalishaji.” – Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo.