Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 24Article 553327

Siasa of Tuesday, 24 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

CCM kutoa kipaumbele kwa walemavu

CCM, kutoa kipaumbele kwa Walemavu CCM, kutoa kipaumbele kwa Walemavu

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema serikali ya awamu ya sita imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kuzingatia kundi la watu wenye ulemavu kwa kulijumuisha, kulishirikisha na kuliwezesha.

Shaka aliyasema hayo jijini Dar es Salaam mbele ya wajumbe na viongozi wa KISUVITA.

Alisema serikali chini ya CCM imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kuhakikisha watu wenye ulemavu wanaheshimiwa, kuthaminiwa, kushirikishwa, kulindwa na wanajumuishwa katika mipango ya maendeleo katika jamii.

Alibainisha kuwa katika bajeti ya mwaka 2021/2022, serikali imetenga sh. bilioni 1.6 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa visaidizi kwa wanafunzi katika shule zote za wenye ulemavu nchini.

“Kundi hili limeendelea kunufaika na fursa ya mikopo isiyo na riba inayotokana na asilimia mbili ya mapato ya ndani ya halmashauri zetu,”