Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 24Article 553492

Habari Kuu of Tuesday, 24 August 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

CDF Mabeyo kwenye ziara ya siku tatu Rwanda

CDF Venance Mabeyo CDF Venance Mabeyo

Leo Mkuu wa Majeshi Jen. Mabeyo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ulinzi nchini Rwanda, Meja Jenerali Albert Murasira na kisha kufanya mazungumzo mwenyeji wake Mkuu wa Majeshi ya Rwanda, Jenerali J Bosco Kazura kwenye Makao Makuu ya Jeshi la Rwanda (RDF), Kimihurura. Akizungumza kutoka Rwanda, CDF Mabeyo amesema ziara hiyo ina lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Jeshi la Ulinzi la Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Rwanda.

Mabeyo ameongeza kuwa ziara ya ya Mkuu wa Majeshi ya Rwanda nchini Tanzania, Jenerali Bosco Kazura ilionesha kuwa nchi hiyo ina Imani kubwa na Tanzania pamoja na ushirika imara wa majeshi hayo. CDF Mabeyo na ugeni wake umetembelea eneo maalum la kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 huko Gisozi, pamoja na kutembelea makumbusho ya mauaji hayo.

Jenerali Mabeyo atatembelea pia Makao Makuu ya Jeshi la Rwanda, Chuo cha Kijeshi pamoja na Kijiji kipya cha kisasa huko Kinigi IDP wilayani Musanze.