Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 13Article 551431

Habari Kuu of Friday, 13 August 2021

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

COVID-19: Wagonjwa 1056 wapata nafuu huku 1437 wakinasa virusi

COVID-19: Wagonjwa 1056 wapata nafuu huku 1437 wakinasa virusi COVID-19: Wagonjwa 1056 wapata nafuu huku 1437 wakinasa virusi

Katika taarifa iliyotolewa Ijumaa, Agosti 13, Wizara ya Afya ilisema jumla ya visa vilivyothibitishwa sasa ni 218,713Wakati uo huo wagonjwa 29 waliripotiwa kupoteza maisha yao kutokana na maradhi hatari ya coronaAidha wagonjwa 1,056 wamepata nafuu kutokana na ugonjwa huoKenya imerekodi visa vipya 1,437 vya COVID-19 kutokana na sampuli 10,764 zilizopimwa katika saa 24 zilizopita ambapo asilimia mpya ya maambizi iiliyorekodiwa 13.4%.

Katika taarifa iliyotolewa Ijumaa, Agosti 13, Wizara ya Afya ilisema jumla ya visa vilivyothibitishwa sasa ni 218,713 huku idadi ya sampuli zilizopimwa tangu kisa cha kwanza cha COVI-19 kuripotiwa ikigonga 2,239,082.

Kati ya wagonjwa wapya 1,377 ni Wakenya, 60 ni raia wa kigeni. Wagonjwa 738 ni wanaume nao 699 ni wanawake. Mgonjwa mwenye umri wa chini ni mtoto wa mwezi mmoja naye mkongwe ana miaka 100.

Visa hivyo vipya vilirekodiwa kama ifuatavyo

Nairobi 496, Nakuru 139, Kiambu 101, Mombasa 100, Murang’a 67, Uasin Gishu 53, Machakos 47, Kajiado 44, Embu 34, Kirinyaga 30, Taita Taveta 28, Kilifi 23, Nandi 22, Kitui 19, Lamu 17, Meru 17, Laikipia 15, Baringo 15,Read also

Watu Wengine 32 Wapoteza Maisha Kutokana na COVID-19, Idadi Jumla ya Vifo kwa Sasa ni 4,273

Marsabit 14, Nyandarua 14, Busia 14, Migori 12, Narok 11, Nyeri 11, Turkana 11, Garissa 10, Kakamega 9, Tharaka Nithi 7, Trans Nzoia 7, Siaya 7,Elgeyo Marakwet 7, Bomet 6, Kisii 6, Tana River 5, Bungoma 4, Vihiga 3, Kericho 3, Homa Bay 2, Isiolo 2, Kisumu 2, Kwale 1, Makueni 1 na West Pokot 1.

Wakati uo huo wagonjwa 29 waliripotiwa kupoteza maisha yao kutokana na maradhi hayo, kati ya miezi ya Aprili hadi Agosti 2021, jumla ya waliofariki dunia imefika 4,302.

Aidha wagonjwa 1,056 wamepata nafuu kutokana na ugonjwa huo ambapo 963 kati yao walikuwa wametengwa manyumbani mwao na 93 wakipokea matibabu katika hospitali mbali mbali nchini.

Jumla ya waliopata nafuu sasa imefika 201,054.

Kwenye zoezi la chanjo linaloendelea, Wizara inasema jumla ya chanjo 1,970,174 hadi sasa zimesambazwa kote nchini.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.