Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 05Article 541120

xxxxxxxxxxx of Saturday, 5 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Chadema kuanza kusajili wanachama kidijitali

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeanzisha mfumo mpya wa usajili wa wanachama wake kidijitali ilikutatua changamoto mbalimbali za kiutendaji na ukusanyaji rasilimali fedha.

Mpango huo ulitambulishwa na Mwenyekiti wa chama Taifa, Freeman Mbowe jana wakati wa kikao cha mashauriano ya viongozi na wanachama wa majimbo ya Ilemela na Nyamagana.

"Kwa zaidi ya miaka thelathini, chama kimekuwa kikikusanya mapato yake kwa mkono lakini mfumo huu utasaidia kukusanya pesa kielektroniki kwa ajili ya kuendeleza shughuli za chama katika majimbo.Tunataka kuhakikisha kabla ya mwaka 2025 tunakuwa na ofisi nyingi katika majimbo na shughuli za chama hazikwami," alisema.

Mfumo huo utakaoanza Julai Mosi mwaka huu, unatajwa kuwa utawezesha kujua nani anaishi Kata ipi na jimbo lipi kwa dhumuni la kutunza kumbukumbu sahihi za wananchama.

Mbowe alitoa wito kwa viongozi wa kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuweza kuandikisha wanachama wengi zaidi.

Alisema chama kitakuwa na kadi za aina tano za uanachama zenye rangi tofauti. Kadi ya bluu itagharimu Sh 2,500, rangi ya fedha Sh 25,000, rangi ya Dhahabu Sh 50,000, rangi ya Platinum Sh 100,000, na rangi ya Almasi Sh 200,000.

Baada ya kanda ya Ziwa, Chadema pia itatambulisha mfumo huo wa kidijitali nchi nzima katika Kanda ya Magharibi, Kati, Nyasa, Kusini, Pwani, Pemba kisha Unguja.

Join our Newsletter