Uko hapa: NyumbaniHabari2021 07 05Article 545548

Habari za Afya of Monday, 5 July 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Chanjo 60 ikiwemo ya Corona zipo kwenye majaribio – TMDA

Chanjo 60 ikiwemo ya Corona zipo kwenye majaribio – TMDA Chanjo 60 ikiwemo ya Corona zipo kwenye majaribio – TMDA

MAMLAKA ya Dawa, Vitendanishi na Vifaa Tiba (TMDA) imesema hadi sasa takribani chanjo 200 ziko kwenye tafiti huku chanjo 60 zikiwa kwenye majaribio ikiwemo ya Corona ambayo wanashirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO), kufanya tathmini na kupata chanjo bora.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa TMDA, Adam Fimbo katika mahojiano maalum na HabariLeo ambapo amesema WHO wanaleta waatalamu katika kuhakikisha ubora na ufanisi wa chanjo hata hizo ikiwemo chanjo ya covid-19 ili kuendana na sera ya kimataifa kuhusu masuala ya chanjo kwa kushirikiana na Wizara ya afya.

“TMDA inahusika katika kuthibitisha ubora wa chanjo ya covid-19 ikiwemo kusajili na kutoa kibali cha uingizaji na kutumika hapa nchini na vilevile kufatilia ufanisi wake,usalama na ubora wake na kutoa elimu kwa umma kuhusu matumizi sahihi ya chanjo.” alisema na kuongeza

“Kuna kamati ya Covid-19 iliyoundwa na mheshimiwa rais ambayo inapendekeza aina ya chanjo, ni chanjo gani ambazo zinaruhusiwa katika nchi kupitia kamati ile imeweza kutoa ushauri tunachosubiri ni utaratibu rasmi kupitia kamati na Wizara ya afya ili kutoa sera, mwelekeo na ni chanjo gani zinaruhusiwa nchini ndio kazi tunayofanya.

Alisema ni kazi kubwa lakini TMDA imejipanga kufanya kazi kuanzia ngazi ya jamii ambayo pia ina wataalamu wa kimataifa kupita WHO kuanza kufahamu hadi sasa kuna chajo ngapi? zilizofanyiwa utafiti na kwa taarifa tu chanjo 200 ziko kwenye tafiti na chanjo 60 ziko kwenye majaribio kwahiyo watafiti duniani pia wanafanya tafiti mbalimbali na udhibiti ndio kazi yao kubwa.

Aidha alisema TMDA kwa sasa kupitia maabara yao inafanya upimaji na kuweza kusoma taarifa za kisayansi na kitaalamu kabla ya kusajili chanjo rasmi ya Corona .