Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 13Article 551407

Habari za Afya of Friday, 13 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Corona Yasababisha Upungufu wa Damu Hospitali

Uhaba wa Damu Hospitali ya Bombo Uhaba wa Damu Hospitali ya Bombo

Hospitali ya Rufaani ya Bombo Mkoani Tanga, inakabiliwa na uhitaji mkubwa wa damu tangu kuibuka kwa mlipuko nwa virusi vya Corona.

Haya yamebainishwa na mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo DK. Naima Yusuph, aliyefafanua kuwa kwa sasa wanategemea damu kutoka hospital ya rufani ya kanda ya KCMC.

"Ugonjwa wa Virusi vya Corona umekuwa tishio kwa wengi waliokuwa wakitoa damu kwa hiari yao, bado uhitaji ya damu kwenye benki ya damu ni kubwa".

Aliongezea kusema kuwa kuna uhitaji mkubwa wa damu salama hospitalini hapo kulinganisha na kiasi wanachopokea cha damu.

"Mahitaji ya damu salama kwa sasa ni zaidi ya lita 60 kwa siku. Tangu mlipuko wa UVIKO-19 ujitokeze na kutangazwa marufuku ya mikusanyiko, kiasi cha uchangiaji damu kimekuwa kidogo"

Ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kuchnagiadamu ili kuokoa maisha ya mama na mtoto.