Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 08Article 584317

Muziki of Saturday, 8 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Country Boy aachana na Konde Gang

Country Boy Country Boy

Rapa anayefanya vyema kunako game ya Bongofleva, Country Boy "Country wizzy" aliekuwa akifanya kazi chini ya Leno ya Konde Gang ameachana na lebo hiyo rasmi leo January 8, 2022.

Kupitia taarifa yake iliyotoka kupitia kurasa zao rasmi za mitando ya Kijamii, Uongozi wa Konde Gang umeandika;

"TAARIFA: Mkataba Kati Ya Konde Music Worldwide Na @countrywizzy_tz Umemalizika Hii Leo Tar 8 January 2022.

Kuanzia Leo Country Wizzy Atakuwa Msanii Anaejitegemea Baada Ya Kufikia Makubaliano Ya Pande Zote Mbili.

Konde Music Worldwide Inamtakia Kila Lenye Kheri Country Wizzy Kwenye Career Yake Ya Music Pamoja Na Maisha Kwa Ujumla"

All the Best Wizzy!!

Je tutarajie Country Boy akisaini kwingine ama atafanya kazi zake chini ya usimamizi wake yeye mwenyewe?

Chini ya Konde Gang, Country Boy alitoa hit songs kama vile Baby, Far away nk