Uko hapa: NyumbaniHabari2021 07 01Article 544885

Habari za Mikoani of Thursday, 1 July 2021

Chanzo: ippmedia.com

DAWASA yatoa elimu ya Majisafi wananchi wa Mgeule,Taliano na Nyeburu

DAWASA yatoa elimu ya Majisafi wananchi wa Mgeule,Taliano na Nyeburu DAWASA yatoa elimu ya Majisafi wananchi wa Mgeule,Taliano na Nyeburu

Mradi wa maji katika kata ya Buyuni umetekelezwa na DAWASA na umehusisha ulazaji wa mabomba kwa umbali wa kilomita 7 katika mitaa mitatu na kugharimu fedha kiasi cha Shilingi Milion 57.5 unategemea kuhudumia wakazi takribani 7,600 wa kata ya Buyuni na maeneo jirani.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyeburu, Mohamedi Gea amehimiza wananchi kujitokeza kupata huduma hiyo kwani walikuwa wanahangaika sana na upatikanaji wa huduma ya majisafi katika kata hiyo kwa miaka mingi.

"Tunawashukuru DAWASA kwa kusikika kilio chetu cha muda mrefu na sasa huduma ya maji imefika mtaani kwetu. Niwaombe wananchi wenzangu kuchangamkia fursa hii ya maunganisho ya Majisafi kwa kufuata taratibu walizotueleza" amesema Gea

Nae msimamizi wa mradi huo kutoka Mkoa wa kihuduma DAWASA Kisarawe, Mhandisi Ermina Audiphas amesema chachu ya Mamlaka ni kuona huduma ya majisafi inawafikia watu wengi zaidi na wamejipanga kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati ili waweze kusogeza huduma zaidi kwa wananchi.

Kwa upande wake afisa maendeleo ya Jamii DAWASA, Elizabeth Eusebius ametoa wito kwa wananchi kuwa walinzi na kutunza miundombinu ya maji ili iwe endelevu na iweze kuhudumia vizazi vijavyo.