Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 13Article 585358

Habari Kuu of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

DC Aingilia Kati Sakata la Nyumba Iliyabomolewa Kisa Deni la Sh 300, 000

DC Aingilia Kati Sakata la Nyumba Iliyabomolewa Kisa Deni la Sh 300, 000 DC Aingilia Kati Sakata la Nyumba Iliyabomolewa Kisa Deni la Sh 300, 000

Siku chache baada ya gazeti la Mwananchi kuripoti juu ya familia ya Nyahure Range kuvunjiwa nyumba kwa kile kinachodaiwa kuwa nyumba hiyo imeshauzwa, Mkuu wa Wilaya ya Ilala (DC), Ng'wilabuzu Ludigija ameiita familia hiyo ofisini kwake pamoja na waliohusika na kuvunja nyumba hiyo.

Akizungumza Jumatano Januari 12, 2021 mmiliki wa nyumba hiyo, Nyahure Range amesema wameagizwa kufika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala kesho kwa ajili ya kusikilizwa.

Nyahure amesema “Mkuu wa wilaya katutaka tukutane ofisini kwake kesho tukiwa na watu wa Kitunda Saccos na Broker (dalali),” amesema Nyahure.

Tukio la nyumba kuvinjwa lilifanyika Januari 6, 2022 ikiwa ni siku chache kabla ya kutolewa kwa hukumu ya Rufaa iliyokatwa na Selina Chacha ambaye ni mke wa Range kutolewa Februari 15 mwaka huu.

Nyumba ilivunjwa kwa kile kilichodaiwa kuwa familia hiyo ilikuwa ikidaiwa Sh300, 000 na Kitunda Saccos huku taarifa ya Kabango General Business ikionyesha kuwa familia hiyo ilitakiwa kuacha nyumba hiyo na mali zao kukamatwa ili kufidia Sh9.9 milioni.