Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 24Article 544078

Habari za Mikoani of Thursday, 24 June 2021

Chanzo: eatv.tv

DC Kheri aagiza mikakati shirikishi ya Elimu Ubungo

DC Kheri James DC Kheri James

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James amesema mijadala inayohusu elimu katika wilaya hiyo haitaangalia kama mwananchi ana elimu kiasi gani au la kwani mikakati inayopaswa kuwekwa kwenye elimu inapaswa kuchangiwa na watu wote kwa faida ya jamii nzima.

Bw. Kheri amesema hayo akiwa kwenye ziara yake katika wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam ambapo amesema vijana wanapaswa kujengewa uwezo ili kukidhi mahitaji katika fursa mabalimbali zinazozalishwa nchini na kuepuka kutengeneza jamii ya wasindikizaji katika maendeleo ya kitaifa.

“Tunapokuja kwenye suala la mikakati ya elimu ni letu sote aliyesoma, ambaye hajasoma, tunapokutana hakuna anaye sema mimi darasa la saba, au Diploma, asiyekuwa na elimu wote tutakuwa na jukumu la kujadili elimu na kupanga mipango bora kwa faida ya watoto wetu,” amesema Kheri.

Aidha, Mkuu wa Wilaya Kheri ametoa onyo asijekutokea mtu yeyote akaanza kuibeza au kuidogolesha elimu kwani elimu ni jambo la msingi na la manufaa kwenye maisha na ukuaji wananchi.

 “Tusikubali lugha za kubeza elimu, kwenye wilaya yetu nikishirikiana na nyie asitokee mtu yeyote iwe ni kwa kisiasa au kwa kiimani kuibeza elimu kama wewe utaki kusoma usisome wewe lakini usitumie jukwaa tunalokupa sisi kuidogosha elimu, kwenye maandiko ya dini watu wanaambiwa waitafute elimu popote ilipo hata kama ni Uchina haiwezekani Mungu aseme kuhusu elimu alafu nyinyi muifanye ndogo” amesema Kheri.