Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 24Article 553348

Habari za Mikoani of Tuesday, 24 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

DC apiga marufuku milegezo, vimini wilayani kwake

Mavazi yasiyo na staha Mavazi yasiyo na staha

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, Kanali Laban Thomas, amezuiya uvaaji wa mavazi yasiyo na staha ikiwemo vimini na suruali za milegezo wilayani kwake na amemuagiza Mkuu wa Kituo cha Polisi wilaya ya Nyasa, kuwakamata na kuwachukulia hatua wale wote watakao vaa mavazi ya namna hiyo.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na kujibu kero za wananchi wa Kijiji cha Lulimbo wilayani humo, ambapo pia akakemea tabia ya wanaume wanaopiga wake zao na kuwataka wabadilike endapo watabainika watachukuliwa hatua za kisheria.

"Wanyasa ni wastaarabu bwana, hata wakiwa wanacheza Mganda wanavaa nguo nyeupe na hazichafuki hata wakicheza masaa na masaa, nguo fupi na Milege Hazitakiwi wilayani Nyasa," amesema Mkuu wa Wilaya.