Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 12Article 551263

Habari za Mikoani of Thursday, 12 August 2021

Chanzo: ippmedia.com

DC apiga marufuku watu wenye ulemavu kukatwa fedha za mikopo

DC apiga marufuku watu wenye ulemavu kukatwa fedha za mikopo DC apiga marufuku watu wenye ulemavu kukatwa fedha za mikopo

Mboneko amebainisha  hayo jana wakati akikagua mradi wa Nguruwe ambao unatekelezwa na watu wenye ulemavu Kitangili Manispaa ya Shinyanga, akiwa ameambatana na Kamati ya Siasa ya chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini.

Alisema baada ya kusikia Taarifa ya watu hao wenye ulemavu, kulalamikia kukatwa fedha za mikopo kiwango ambacho wanakiomba Halmashauri na kupewa fedha Nusu, hali ambayo inakwamisha kufikia malengo yao, na kuagiza kuanzia sasa Marufuku watu hao kukatwa fedha ambazo huziomba.

“Naagiza kuanzia sasa Marufuku watu wenye ulemavu kukatwa fedha za mikopo asilimia mbili ambazo wanaziomba, bali wapewe kiwango sahihi, sababu ni kundi maalumu harafu wapo wachache, na mkikatwa tena fedha zenu nipeni taarifa,” alisema Mboneko

Naye, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Abubakari Mukadam, ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kutoa fedha za Mikopo kwa watu wenye ulemavu, ili kuwainua kiuchumi sababu kundi hilo mara nyingi hua linasahaurika.Awali Mwekahazina wa kikundi hicho cha watu wenye ulemavu Janety Maganga, akisoma taarifa, alisema kikundi chao kina watu Wanne ambapo wanajihusisha na ufugaji wa Nguruwe, na waliomba fedha za mikopo Sh. milioni 5, lakini wakapewa Sh, Milioni 3, fedha ambazo wamedai kutokidhi mahitaji yao.