Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 14Article 542584

Habari Kuu of Monday, 14 June 2021

Chanzo: eatv.tv

DCI Wambura awatumia salamu wahalifu

DCI Wambura awatumia salamu wahalifu DCI Wambura awatumia salamu wahalifu

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) Camilius Wambura amesema Jeshi la Polisi halitamvumilia mtu yeyote atakayeendelea kujihusisha na vitendo vya uhalifu, kauli ambayo ameitoa  wakati huu ambao Jeshi hilo linaendelea na operesheni kali ya kupambana na vitendo hivyo.

Submitted by Elbogast on Ijumaa , 11th Jun , 2021 Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) Camilius Wambura

DCI Wambura ameyasema hayo leo Jijini Dodoma katika kikao kazi kilichowashirikisha Maofisa wa Makao Makuu ya Upelelezi na Wakuu wa Upelelezi wa mikoa nchini kwa lengo la kupanga mikakati ya kupambana na uhalifu pamoja na kutathmini hali ya uhalifu nchini.

Amesema mtu yeyote amabaye anajihusisha na vitendo hivyo kuacha mara moja kwa kuwa mkono wa Jeshi la Polisi ni mkubwa na kwa wakati huu hakuna upenyo wowote utakaoachwa kwa kuwa operesheni inaendelea nchi nzima.

“Wito wangu kwa wahalifu ni bora watafute kazi nyingine ya kufanya kwa kuwa hatuna huruma kwa watu hao na wananchi waendelee kutupatia taarifa zao ili tuhakikishe nchi yetu inaendelea kuwa salama,” amesema DCI Wambura.

Kwa upande wake Naibu DCI, DCP Faustine Shilogile amesema Idara ya Upelelezi wa makosa ya Jinai Makao Makuu inaendelea kuboresha mifumo ya ukusanyaji wa takwimu na utoaji wa mafunzo kwa watendaji wa idara hiyo ili kuwa na wapelelezi wenye weledi ambao watasaidia kuharakisha upelelezi wa kesi zinazoripotiwa katika vituo vya Polisi.