Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 13Article 551386

Habari Kuu of Friday, 13 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Daktari Bingwa wa watoto nchini Afariki dunia

Daktari, Augustine Massawe Daktari, Augustine Massawe

Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Augustine Massawe amefariki dunia leo katika hospitali hiyo,

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma Muhimbili, Aminiel Aligaesha amethibitisha kutokea kwa kifo cha Daktari huyo huku akieleza kuwa alikuwa akikabiliwa na tatizo la upumuaji.

Dk.Massawe, alisifika kwa weledi wake mkubwa aliokuwa nao wa kutibu watoto wenye matatizo sugu ya kiafya.