Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 22Article 573313

Habari za Afya of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Dk.Gwajima aagiza akiba ya maji Muhimbili

Dk.Gwajima aagiza akiba ya maji Muhimbili Dk.Gwajima aagiza akiba ya maji Muhimbili

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk, Dorothy Gwajima amevitaka vituo vya afya kutafuta mbinu mbadala ya kuweka akiba ya maji ili kukabiliana na hali ya upungufu wa huduma hiyo.

Dk Gwajima ametoa agizo hilo alipofanya ziara ya kushtukiza katika Hospital ya Taifa Muhimbili ambako kunahitajika zaidi ya lita 60,000 za maji ili kuendelea kuhudumia wagonjwa.

Aidha, Dk Gwajima amefikia uamuzi huo baada ya malalamiko ya wananchi kukosa huduma ya maji katika hospitali hiyo.

Kufuatia hali hiyo, Dk Gwajima ameagiza uongozi wa hospitali hiyo na zote nchini kununua vifaa vya kuhifadhi maji zaidi ya lita 120 ili kuwe na akiba itakayokabiliana na changamoto hiyo.