Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 21Article 573220

Habari za Afya of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Dk Gwajima kuwachulia hatua watumishi wasiokuwa na maadili

Dk Gwajima kuwachulia hatua watumishi wasiokuwa na maadili Dk Gwajima kuwachulia hatua watumishi wasiokuwa na maadili

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dk Dorothy Gwajima amesema hatasita kuwachukulia hatau watumishi wanaokiuka maadili kwa kufanya biashara ya kuuza damu ambapo ni kinyume cha sheria.

Dk Gwajima amesema hayo wakati wa zoezi la uchangiaji damu kutoka makundi ya vijana wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi na utoaji wa chanjo za UVIKO 19.

Tamasha hilo limeandaliwa na kijana aliyetupwa vichakani na kutelekezwa na wazazi wake anayeishi mazingira magumu na hatarishi James Fondation kwa kushirikiana na Serikali wanahamasisha jamii kuchangia damu salama kwa manufaa ya Taifa.

Dk Gwajima amesema kuwa Mpango wa Taifa wa Damu Salama hutoa damu bila malipo kwa hospitali zote, hivyo wagonjwa wote wanatakiwa kupata tiba ya damu bila malipo yoyote.

Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Serikali kwa kuwafichua watumishi wanaouza damu salama kwenye vituo vya afya ili wawajibishwe kisheria

Aidha, Dk Gwajima ametoa siku 30 kwa taasisi ya kuratibu mpango wa Taifa wa Damu Salama kushirikisha wadau wengine wote wakiwemo Chama cha Msalaba Mwekundu kuhakikisha kinatafuta namna ya kuratibu upatikanaji wa damu salama zaidi ya chupa 550,000 zitakazo tosheleza mahitaji ya hospitali na vituo vya afya hapa nchini ili kunusuru vifo vya wagonjwa vinavyosababishwa na upungufu wa damu.

Amesema kuwa maisha ya mwanadamu yanategemea damu salama ambapo kundi kubwa la watoto chini ya miaka mitano wanahitaji damu kwa asilimia 50 ikifatiwa na kundi la mama wajawazito aslimia 30, ajali mbalimbali ikiwemo waendesha pikipiki bodaboda asilimia 15 na asilimia 5 hupelekwa kwa wagonjwa wa saratani na upasuaji mkubwa wa moyo.

Dk Gwajima amesema kuwa shirika la afya Duniani linapendekeza kuwa ili nchi iweze kukusanya damu ya kutosha inapashwa kukusanya chupa za damu kutoka kwa asilimia moja ya idadi ya watu katika taifa ambapo hapa nchini inatakiwa kukusanya damu chupa kumi kati ya watu 1000,

Amesema kuwa mpango wa Taifa wa Damu umeweka malengo ya kukusanya damu salama chupa 550,000 ambapo vijana wamekuwa mstari wa mbele kujitolea kutoa damu inayokusanywa hapa nchini kwa asilimia 80 ila kutokana na hamasa ndogo ya wananchi zinakusanywa chupa 312,907 sawa na chupa sita kwa watu 1000.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratan Ocean Road Dk Julius Mwaiselage amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia fedha taasisi ya Ocean Road Kiasi cha Sh bilioni 5.4 kwa ajili ya kuboreha huduma ya afya ikiwemo kununua mashine ya MRI na kuanzisha kitengo cha ICU.

Kwa upandewake Mkurugenzi Mtendaji wa James Fondation James Yusta ameimba serikali kuanzisha Mfumo wa elimu ya malezi bora katika shule za msingi,sekondari na vyuo ili kuandaa watoto kuwa wazazi na walezi bora katika familia kwa lengo la kutokomeza wimbi la watoto wanaoishi katika mazingira