Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 16Article 557986

Habari Kuu of Thursday, 16 September 2021

Chanzo: ippmedia.com

Dk. Kijaji avipiga mkwara vyombo vya habari

Dk. Kijaji avipiga mkwara vyombo vya habari Dk. Kijaji avipiga mkwara vyombo vya habari

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk.Ashatu Kijaji amesema hatakuwa tayari kuvumilia vyombo na waandishi wa habari watakaochapisha taarifa za kutaka kulichafua taifa.

Waziri Ashantu ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akifungua Mafunzo ya Kamati ya Ukaguzi ya Wizara hiyo, jijini Dodoma.

"Lazima katika utendaji kazi wa waandishi wa habari watangulize uzalendo kwa Taifa."

"Niwahakikishie sitakuwa mvumilivu kwa yeyote atakayejaribu kufanya hivyo kuandika habari zenye viashiria vya uvunjifu wa amani tutachukua hatua," amesema.