Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 14Article 557473

Habari Kuu of Tuesday, 14 September 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Dk Mabula asikitishwa ucheleweshaji wa fedha miradi NHC

Dk Mabula asikitishwa ucheleweshaji wa fedha miradi NHC Dk Mabula asikitishwa ucheleweshaji wa fedha miradi NHC

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula amesikitishwa na kusuasua kwa utekelezaji wa miradi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wilayani Chato mkoani Geita hali inayosababishwa na ucheleweshaji wa fedha.

Dk Mabula amesikitishwa na hali hiyo alipotembelea na kukagua miradi mitatu inayotekelezwa na NHC ambayo ni mradi wa mnada wa mifugo Buzirayombo wenye thamani ya Sh bilioni 4.8, mradi wa ujenzi wa shule maalumu ya Mbuye bilioni 5.14 na mradi wa nyumba 20 za watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda- Chato wa thamani ya Sh bilioni 1.139.

Akizungumza mara baada ya kukagua miradi yote mitatu leo tarehe 14 Septemba 2021 akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani humo, Dk Mabula alisema miradi hiyo ni muhimu na inapaswa kukamilika kwa wakati ili ianze kutumika.

"Haitakuwa na maana Serikali kuwekeza fedha nyingi kwenye miradi wa mnada wa mifugo, shule maalum na nyumba za watumishi wa sekta ya afya na kuachwa bila kukamilika jambo ambalo halitaleta maana". alisema Dkt Mabula.

Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Kagera Maneno Mahenge alimwambia Naibu Waziri wa Ardhi Dk Mabula kuwa shirika lake la NHC limekuwa likisuasua kutekeleza kwa kasi miradi katika wilaya hiyo kutokana na kutopatiwa fedha za miradi kwa wakati.