Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 25Article 559678

Habari Kuu of Saturday, 25 September 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Dk Mpango: "Niliogopa sana, ila nchi ipo salama"

Dk Mpango: Dk Mpango: "Niliogopa sana, ila nchi ipo salama"

MAKAMU wa Rais Dk Philip Mpango amesema kipindi ambacho Rais Samia Suluhu hayupo nchini alikuwa anaogopa uwenda likatokea la kutokea.

Dk Mpango ameyasema hayo muda mfupi baada ya kumpokea Rais Samia Suluhu, uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere akitokea New York Marekani alipokwenda kushiriki mkutano wa 76 wa Baraza la Umoja wa Mataifa (UNG)

“ Nchi yako ipo shwari, ipo salama imetulia kama maji kwenye mtungi, kipindi chote ambacho haupo nilikuwa naogopa, likitokea jambo la kunitisha nitafanyaje, lakini naomba nikuhakikishie nchi yako ipo salama, nawashukuru watanzania kwa kuendeleza utulivu.” amesema Dk Mpango

Aidha, Dk Mpango amempongeza Rais Samia kwa namna alivyoibeba Tanzania kwa kusoma hotuba nzuri katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kwa kutulia.

“Naomba nikupongeze umetubeba, umetuwakilisha vizuri, sisi ambao tumepata nafasi ya kukaa kwenye kile chumba cha kimataifa, umetubeba sana, umetulia, umesoma vizuri hotuba,” amesema