Uko hapa: NyumbaniHabari2021 07 01Article 544933

Habari Kuu of Thursday, 1 July 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Dk Mpango aomba Tanzania itangazwe Ufaransa 

Dk Mpango aomba Tanzania itangazwe Ufaransa  Dk Mpango aomba Tanzania itangazwe Ufaransa 

MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango amewaomba maseneta wa Ufaransa watangaze mazuri ya Tanzania na waunge mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kutekeleza miradi ya maendeleo.

Alitoa kauli hiyo jana jijini Paris alipokutana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Kundi la Maseneta wa nchi hiyo ambao ni marafiki wa Tanzania, Ronan Dantec.

Dk Mpango alieleza jitihada na mafanikio ya serikali kuwa ni pamoja na nchi kufikia uchumi wa kati, utekelezaji wa miradi ya kimkakati ukiwemo ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere litakalozalisha megawati 2,115,

Seneta Dantec alieleza kufurahishwa na uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Ufaransa na kuahidi kuendelea kuisemea Tanzania ili kusaidia kuvutia wawekezaji na watalii zaidi kutoka nchini humo.

Viongozi hao pia walijadili kuanzisha ushirikiano kati ya Jiji la Dodoma na Jiji la Paris na kueleza kuwa ushirikiano huo utajikita kwenye miradi yakiwemo matumizi bora ya ardhi, usafiri wa umma, nishati, pamoja na miradi mingine inayolenga kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.

Seneta Dantec alizungumzia pia umuhimu wa kuendelea kuhifadhi mazingira ili kupunguza hewa ya ukaa duniani, huku akishauri kuwepo na mfuko wa fidia kwa watakaoathirika na masuala ya kuhifadhi na kulinda mazingira.

Dk Mpango alitembelea pia maktaba iliyopo katika jengo la Seneta na kujionea historia iliyohifadhiwa vizuri ya kuona taarifa za mpangilio wa safu ya uongozi uliowahi kutawala nchini humo. Alitembelea pia ukumbi wa mikutano ya Bunge la Seneti.

Dk Mpango yuko Ufaransa kuhudhuria Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa lililoanza jana na litakwisha kesho. Jukwaa hilo lina lengo la kuhamasisha haki za usawa wa kijinsia kama zilivyokubaliwa katika mkutano wa Beijing mwaka 1995.