Uko hapa: NyumbaniHabari2021 07 03Article 545104

Habari Kuu of Saturday, 3 July 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Dk Mpango ashukuru mchango wa Ufaransa

Dk Mpango ashukuru mchango wa Ufaransa Dk Mpango ashukuru mchango wa Ufaransa

MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa, Marie-Hellen Loison yaliyojikita kujadili masuala mbalimbali ya kukuza na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na shirika hilo

Dk Mpango alishukuru shirika hilo kwa kwa kuendelea kutoa ufadhili kwa Tanzania kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya maji, usafi wa mazingira, nishati, elimu na utalii.

Naibu Mkurugenzi Mkuu huyo alisema shirika hilo limepandisha hadhi ya ofisi yake jijini Dar es Salam kuwa ofisi ya kudumu tangu mwaka 2018 na lipo kwenye mchakato wa kufungua Ofisi ndogo jijini Dodoma kuwa karibu na Wizara/Taasisi mbalimbali za Serikali ambazo inashirikiana nazo.

Alisema shirika hilo limedhamiria kupanua wigo wa ushirikiano wake na Tanzania ikiwa ni pamoja na kuibua maeneo mapya ya kuendeleza ushirikiano.

Alisema wameweka nia ya kuwekeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa katika masuala ya uchumi wa Bluu, utunzanji wa mazingira,kilimo pamoja na kutilia mkazo masuala ya kijinsi .

Dk Mpango alishukuru shirika hilo kwa kuchagua maeneo muhimu yanayogusa maisha ya wananchi wa kawaida moja kwa moja.

Alimfahamisha Naibu Mkurugenzi Mkuu kuwa maeneo hayo pia ni vipaumbele vya serikali ambayo yameainishwa katika Mpango wa Tatu wa Maendeleo uliozinduliwa hivi karibuni.

Aliainisha sekta ambazo zimeendelea kuwa za kipaumbele ikiwa ni pamoja na miundombinu, nishati, kuboresha miundombinu ya maji ambazo zitasaidia kuchochea Tanzania ya Viwanda ambayo ilikuwa moja ya malengo ya Mpango wa Pili wa Maendeleo (FYDP II).

Aidha, kutokana na umuhimu wa shirika hilo kwa Tanzania, Makamu wa Rais alimhakikishia ushirikiano wa Serikali ya Awamu ya Sita katika kutekeleza majukumu ya shirika hilo nchini.