Uko hapa: NyumbaniHabari2021 10 13Article 563047

Habari Kuu of Wednesday, 13 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Dk. Mpango atembelea mradi wa JNHPP

Dk. Mpango atembelea mradi wa JNHPP Dk. Mpango atembelea mradi wa JNHPP

Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango amepongeza hatua za ujenzi wa mradi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP) baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ya mradi huo Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani akiwa ameambatana na Waziri wa Nishati, January Makamba, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge na Viongozi wengine.

Maeneo aliyotembelea ni pamoja na ujenzi wa tuta kuu la bwawa, njia za kupeleka maji kwenye mitambo itakayofua umeme, jengo la mitambo pamoja na kituo cha kupokea na kusafirisha umeme.

"Waziri wa Nishati pamoja na TANESCO nawapongeza kwa kuendelea kusimamia ujenzi wa mradi huu, mnafanya kazi nzuri sana, Serikali inawapongeza sana na jicho la Serikali liko hapa kwani tuliwaahidi Watanzania kwamba tutaujenga mradi huu ili tupate umeme wa kutosha utakaojenga uchumi wa viwandaā€¯ Amesema Dk. Mpango.