Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 23Article 553030

Habari Kuu of Monday, 23 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Dk Mpango kuongoza kikao kero za Muungano

Dk Mpango kuongoza kikao kero za Muungano Dk Mpango kuongoza kikao kero za Muungano

MAWAZIRI na makatibu wakuu wa wizara katika serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) wanatarajiwa kukutana Zan- zibar leo kutafuta suluhisho la changamoto zinazolalamikiwa na wananchi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Dk Saada Mkuya jana waliwaeleza waandishi wa habari kuwa, kesho Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango atatangaza matokeo ya mkutano huo.

“Wote tunakutana kesho (leo) katika ukumbi wa Idris Abdulwakil kabla ya kutembelea jengo la 3 la abiria katika Uwanja wa Ndege

Zanzibar na kiwanda cha maziwa cha Aam kwa sababu hivi karibuni haya maeneo yamekuwa yakilalamikiwa kuhusu Muungano” alisema Jafo katika ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mtaa wa Vuga katika eneo la Stone Town.

Alisema Dk Mpango ataongoza kikao cha mawaziri na makatibu wakuu na kikao cha mwisho kabla ya kutangaza matokeo na kwamba pia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdalla watahudhuria.

Jafo kesho mchana atasainiwa makubaliano ya kikao hicho na kwamba Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi wamedhamiria changamoto na malalamiko katika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar vinapungua.

Alisema kulikuwa na kero 25 za Muungano na saba kati ya hizo zilipatiwa ufumbuzi. Oktoba mwaka jana kero tano za Muungano zilipatiwa ufumbuzi ikiwemo ya kuihusisha Zanzibar kwenye masuala ya kimataifa, ushiriki wa Zanzibar katika masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kodi za bidhaa zinazotolewa Zanzibar kupelekwa Tanzania bara, utafutaji wa mafuta na gesi, na namna ya kujadili na kutafuta ufumbuzi wa migogoro na malalamiko katika Muungano.

“Sasa tunazifanyika kazi 18 zilizobaki, tunatumaini baada ya majadiliano ya Jumatatu na Jumanne tutazimaliza ”alisema Jafo.

Dk Mkuya alisema walikuwa na furaha kwa sababu wamekuwa wakipata ufumbuzi wa kero kwa amani.

“Tunaomba Watanzania wote wawe na subira na waziamini serikali zote” alisema.