Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 30Article 560506

Diasporian News of Thursday, 30 September 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Dk Mwinyi: Sina ubaguzi kuteua viongozi

Dk Mwinyi: Sina ubaguzi  kuteua viongozi Dk Mwinyi: Sina ubaguzi kuteua viongozi

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema aliapa kuwatumikia wananchi wote hivyo hana ubaguzi kutokana na jinsi, dini au rangi ya mtu.

Akizungumza na viongozi wa dini ya Kikristo huko Welezo mjini Unguja, Dk Mwinyi alisisitiza kwamba uteuzi wa viongozi haufanyiki kwa misingi ya dini, jinsi au rangi ila vigezo na sifa.

Alisema yupo tayari kupokea majina ya vijana wenye sifa ambao wana uwezo wa kuongoza serikalini.

‘’Nileteeni majina ya vijana wenye uwezo na sifa za kielimu ili tuwachague kushika nafasi mbalimbali za uongozi...

Vigezo vya uteuzi wa nafasi mbalimbali za uongozi sifa yake kubwa ni uwezo na sio misingi ya dini au kabila la mtu au anatoka wapi, iwe kusini au kaskazini,’’ alisema Dk Mwinyi.

Alisema hayo wakati akijibu malalamiko ya viongozi wa dini ya Kikristo kuhusu uteuzi wa nafasi za uongozi ikiwemo za kisiasa wakidai kuwa hazitolewi kwa makundi mengine ya dini.

Aliwataka viongozi wa dini waunge mkono serikali ya umoja wa kitaifa ambayo imeondoa malumbano ya kisiasa na kuondosha mivutano iliyojenga chuki na uhasama.

Dk Mwinyi alisema hatua iliyofikia sasa hakuna sababu kwa nini wananchi washindwe kuyafikia malengo yaliyowekwa ikiwemo uchumi wa buluu na uwekezaji.

‘’Serikali ya umoja wa kitaifa imewaunganisha wananchi wote na kwa kiasi kikubwa kuondosha malumbano ya kisiasa na uhasama... Nashukuru sana hatuna sababu kwa nini tushindwe kuyafikia malengo tuliyojiwekea kwa sababu amani tunayo na utulivu wa kidini,’’ alisema.

Katika malalamiko yaliyowasilishwa na kiongozi wa Kanisa la Kilutheri (KKKT), Dayosisi ya Zanzibar, Askofu Shukuru Maloda alisema Wakristo wanapata vikwazo na kukataliwa wakati wanapotaka kujenga nyumba za ibada katika ardhi zao wanazozimiliki kihalali.

Dk Mwinyi alisema hakuna vikwazo kwa waumini wa dini ya Kikristo wakati wanapotaka kujenga nyumba za ibada katika maeneo yao au ardhi zao kukataliwa au kuzungushwa bila ya kupewa maelezo yanayofahamika.

‘’Wakati mwengine mkiona mnabanwa au mnakataliwa kufanya shughuli zenu ikiwemo ujenzi wa nyumba za ibada na watendaji ambao sio waaminifu wanaofanya hivyo kwa misingi ya ubaguzi basi nioneni mimi moja kwa moja,’’ alisem