Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 19Article 543421

Dini of Saturday, 19 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Dk Mwinyi: Waliokusudia kwenda hija wajipange mwakani

Dk Mwinyi: Waliokusudia kwenda hija wajipange mwakani Dk Mwinyi: Waliokusudia kwenda hija wajipange mwakani

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi amewaeleza wananchi wa Zanzibar kwamba mwaka huu kama ilivyokuwa mwaka jana hapatakuwa na fursa ya kwenda kuhiji Makka kwa waumini walio kusudia kufanya ibada hiyo, badala yake wajipange kwa mwakani.

Alisema hayo jana alipokuwa akitoa salamu zake kwa waumini wa dini ya Kiislamu baada ya Sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Nour, Unguja Ukuu Kae Pwani, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.

Mwinyi alisema kutokana na taarifa iliyotolewa na Serikali ya Saud Arabia inayosema kuwa kwa hali ya ugonjwa wa COVID 19 bado mwaka huu hawatoruhusu mahujaji kutoka nje na watakaoruhusiwa ni raia na

wageni wanaoishi nchini humo.

“...lakini kama tunavyoambiwa na Masheikh kwamba jambo ukishalitilia nia basi Mwenyezi Mungu anakuandikia thawabu zake...basi tunamuomba Mwenyezi Mungu wale wote waliotia nia mwaka jana na mwaka huu wawe wamepata thawabu za kuhiji kama walivyokuwa wametia nia,” alisema.

Mwinyi aliwataka wana siasa, viongozi wa dini pamoja na

vyombo vya habari kuhakikisha kauli zao zinajenga amani kwani kinyume chake, zinaweza kuiondosha amani iliyopo.

Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Shehe Khalid Ali Mfaume aliwaeleza waumini hao wa Unguja Ukuu kwamba Mwinyi amekuwa na hekima kubwa jambo ambalo linajidhihirisha anavyowapenda wananchi wake kwa kushirikiana nao katika sala za Ijumaa katika misikiti mbali mbali a nchini.