Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 27Article 554005

Diasporian News of Friday, 27 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Dk Mwinyi aipongeza SADC ulinzi wa amani

Dk Mwinyi aipongeza SADC ulinzi wa amani Dk Mwinyi aipongeza SADC ulinzi wa amani

RAIS wa Zanzibar, Dk Hussein Mwingi amepongeza ushirikiano uliopo kati ya nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) katika suala zima la kulinda amani.

Dk Mwinyi aliyasema hayo Zanzibar jana alipokutana na kuzungumza na Mwakilishi wa Jamhuri ya Msumbiji nchini Tanzania, Balozi Rocardo Amrosio Mtumbuida aliyefika kujitambulisha Ikulu, Zanzibar.

Kwa upande wake, Balozi Amrosio alitoa pongezi kwa Rais Mwinyi kwa ushindi alioupata katika Uchaguzi Mkuu uliopita uliofanyika mwaka jana na kushika wadhifa huo wa Rais wa Zanzibar.

Katika hatua nyingine, Dk Mwinyi alikutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Pakistan nchini Tanzania, Balozi Muhammad Saleem.

Katika kikao hicho viongozi hao walizungumzia masuala mbalimbali ya kimaendeleo na uhusiano wa kibiashara baina ya Pakistan na Zanzibar.

Akizungumzia mazungumzo hayo, Dk Mwinyi alisema kuna umuhimu wa Pakistan kuendelea kushirikiana na wafanyabiashara wa Zanzibar katika sekta binafsi kupitia Jumuiya ya Wafanyabiashatra wenye Viwanda na Wakulima kwa kutembelea kuimaisha uhusiano na fursa za kibiashara.

Kwa upande wake, Balozi Saleem alisema Zanzibar inaweza kunufaika kwa kiasi kikubwa na Pakistan kutokana na ushirikiano uliopo wa kibalozi kupitia sekta za elimu, uchumi wa buluu, biashara pamoja na fursa za masomo.

Wakati huohuo, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amefanya uteuzi wa wakurugenzi na Mthamini Mkuu wa Serikali katika Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Zena Saidi, Rais Mwinyi amemteua Muchi Juma Ameir kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji.

Saidi alisema pia Rais Mwinyi amemteua Juma Ameir Mgeni kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Upimaji na Ramani, Khamisyy Hamid Mohamed kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Utumishi na Tahir Mussa Omar ameteuliwa kuwa Mthamini Mkuu wa Serikali. Uteuzi wa viongozi hao umeanza rasmi jana.