Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 30Article 540640

Diasporian News of Sunday, 30 May 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Dk Mwinyi aitaka misikiti kusaidia kutatua changamoto za kijamii

Dk Mwinyi aitaka misikiti kusaidia kutatua changamoto za kijamii Dk Mwinyi aitaka misikiti kusaidia kutatua changamoto za kijamii

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi, ameitaka kamati za misikiti kushirikiana na waumini katika utatuzi wa changamoto zinazoikabili jamii.

Alitoa mwito huo juzi katika ufunguzi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Taqwa uliopo Bambi, Mkoa wa Kusini Unguja, uliojengwa kwa ushirikiano kati ya wananchi na mfadhili.

Aliwataka waumini hao kutumia msikiti huo kama kituo cha kujifunza na kuzungumzia matatizo

yanayoikabili jamii, kama vile changamoto za maisha zinazowahusu yatima, wajane pamoja na vitendo vya udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto.

Alisema mbali na ibada ya swala, pia kuna umuhimu wa kuendeleza na kutumia msikiti huo katika mambo mbali mbali, kwa mujibu wa mafunzo ya Mtume Muhammad (SAW). Alisisitiza umuhimu wa waumini

wa msikiti huo kuutunza udumu miaka mingi.

Aidha, aliwaeleza waumini hao wajibu walionao katika kufanya mambo mema ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya akhera yao, akibainisha kila muumini ana nafasi ya kuimarisha msikiti huo katika matunzo, ikiwemo kusaidia huduma za maji, umeme au kuufanyia matengenezo madogo madogo.

Aidha Dk Mwinyi alipongeza juhudi za waumini wa kijiji hicho kwa kuunganisha nguvu zao na kuanza kazi ya ujenzi wa msikiti huo mkubwa badala ya kusubiri mfadhili.

Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja Rashid Hadidi, alimshukuru Dk Mwinyi kwa kujumuika pamoja na waumini wa msikiti huo katika hafla hiyo muhimu ya ufunguzi wa msikiti, sambamba

na kuishukuru Kamati ya Msikiti na Msimamizi wa ujenzi kwa kukamilisha kazi hiyo kwa ufanisi.

Naibu Kadhi wa Zanzibar, Shehe Othman Hassan Ngwali aliwataka waumini wa msikiti huo kujiimarisha kwa njia mbalimbali, ikiwamo ya kutumika kwa shughuli za kujifunza.

Akisoma risala ya waumini wa msikiti huo, Shehe Omar Abdalla, alisema ujenzi

wa msikiti huo wenye uwezo wa kuswaliwa na waumini wapatao 2,000, umejengwa baada ya ajali ya moto kwa msikiti wa mwanzo miaka minne iliyopita.

Shehe Omar kwa niaba ya Kamati ya Msikiti huo alitoa shukurani kwa waumini wote waliosaidia na kufanikisha ujenzi wa msikiti huo pamoja na kutoa ahadi ya kuutunza na kutumika kwa misingi iliyokusudiwa.

Join our Newsletter