Uko hapa: NyumbaniHabari2021 07 06Article 545641

Habari Kuu of Tuesday, 6 July 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Dkt. Mpango Aipongeza Global Publishers

Dkt. Mpango Aipongeza Global Publishers Dkt. Mpango Aipongeza Global Publishers

MAKAMU wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango ameipongeza Kampuni ya Global Publishers & Enterprises Ltd wachapishaji wa magazeti ya Championi, SpotiXtra, Ijumaa, Risasi, Uwazi, Amani na Ijumaa Wikienda kwa kudhamini maonyesho ya 45 ya biashara Kimataifa maarufu kama Maonyesho ya Sabasaba.

Dkt. Mpango ametoa kauli hiyo leo Jumatatu, Julai 5, 2021 wakati akihutubia Taifa katika ufunguzi wa maonyesho hayo huku akizitaja kampuni na taasisi nyingine pia ambazo zimedhamini maonyesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Nawashukuru TANTRADE kwa kumualika Mhe. Rais Samia Suluhu kuwa mgeni rasmi kwenye maonyesho haya ya 45 ya Sabasaba, alipenda sana kushiriki maonyesho haya lakini kutokana na majukumu ya Kitaifa aliyoayo Dodoma ameshindwa hivyo akaniomba nije kumuwakilisha.

“Nawapongeza TANTRADE na wadau wote wa biashara na maendeleo kwa kuandaa maonyesho haya.

“Nawapongeza sana wadhamini wa maonyesho haya; NBC, Vodacom, Tigo, CRDB, TIRA, NIC, TSN, Kings Lion, TANESCO, NSSF na Global Publishers Ltd, nawashukuru kwa jinsi mlivyojitoa, asanteni sana.

“Licha ya changamoto ya janga la Corona lakini nyingi zimekuja kushiriki maonyesho haya, hii inaonyesha ushirikiano mkubwa uliotengenezwa na uongozi wa awamu zote wa Tanzania katika nyanja mbalimbali ikiwemo kukuza biashara na uwekezaji.” amesema Dkt. Mpango.

Share this:TweetWhatsApp Related