Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 11Article 585004

Habari Kuu of Tuesday, 11 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Dkt. Mpango Ashiriki Ibada Malawi

Dkt. Mpango Ashiriki Ibada Malawi Dkt. Mpango Ashiriki Ibada Malawi

Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango na mke wake Mboni Mpaye Mpango leo asubuhi wameshiriki Ibada katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Patrick iliopo mtaa wa 11, Lilongwe Nchini Malawi.

Dk Mpango yupo Malawi kumuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) unaofanyika tarehe 11-12 Januari 2022.