Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 19Article 572776

Habari Kuu of Friday, 19 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Dkt.Mpango, wawekezaji wajadili mazito Singapore

Philip Mpango, Makamu wa Rais Philip Mpango, Makamu wa Rais

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Wafanyabiashara na wawekezaji wa Nchi ya Singapore, mazungumzo hayo yamefanyika katika Hoteli ya Shangri La nchini Singapore.

Wafanyabiashara hao wamemueleza Makamu wa Rais nia yao ya kuwekeza nchini na kuiomba serikali kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji ikiwemo kuondoa vikwazo hasa katika masuala ya biashara ya kilimo,

Aidha wameomba juhudi ziongezwe kwenye kuimarisha ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali pamoja na kuomba kuendelea kuimarika kwa ushirikiano baina ya Tanzania na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kurahisisha upatikanaji wa masoko ya bidhaa zitakazozalishwa.

Akizungumza na wafanyabishara hao Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ametaja hatua zinazochukuliwa na serikali katika kuweka mazingira salama ya uwekezaji yatakayo wavutia zaidi kuwekeza.

Ametaja maboresho hayo kuwa ni pamoja na kuendeleza miradi mikubwa itakayotoa unafuu katika kuwekeza kama vile Ujenzi wa mradi wa Umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (JNHPP), Ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR),Kuboresha shirika la ndege ambapo mpaka sasa jumla ya ndege 11 zimekwisha nunuliwa,kuboresha bandari, kuwekeza katika kutoa nishati vijijini, kuboresha miundombinu pamoja na huduma za kijamii.