Uko hapa: NyumbaniHabari2021 10 06Article 561682

Habari za Afya of Wednesday, 6 October 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Dozi milioni 1 za COVID-19 zitakua zimeisha kabla ya muda wa kuharibika" - Serikali

Dozi milioni 1.05 ya Johnson & Johnson kutumika kabla ya Disemba Dozi milioni 1.05 ya Johnson & Johnson kutumika kabla ya Disemba

Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema kuwa chanjo aina ya Johnson & Johnson milioni 1.058 zilizotolewa na Serikali ya Marekani zitamalizikia kutumika kabla ya mwezi Disemba.

Haya yamethibitishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Prof Abel Makubi aliyebainisha kuwa idadi ya watu wanaojitokeza kupata chanjo hiyo imeongezeka kutoka watu 3000 hadi 5000 kwa siku kufuatia kampeni zinazoendelea nchi nzima.

"Kampeni za chanjo zimesaidia sana kuongeza idadi ya watu wanaojitokeza kila siku, sasa watu wana elimu ya kutosha , na wanapokea chanjo nchi nzima na dozi zote zitatumika kabla ya tarehe ya kuharibika ambayo ni mwezi Disemba 2021" Amesema Katibu huyo.

Zoezi la utoaji chanjo kitaifa lilianza mwezi Agosti lilipozinduliwa rasmi na Rais Samia, hata hivyo Serikali ilianzisha kampeni mpya ya kitaifa ya utoaji chanjo kwa kuwaelemisha wananchi juu ya umuhimu wa kupata dozi hiyo mara baada ya Rais Samia kusema hadharani kuwa hajafurahishwa na muitikio wa zoezi hilo kitaifa.