Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 24Article 559387

Habari za Mikoani of Friday, 24 September 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Dr. Mpango aagiza January, bosi Tanesco waende Kigoma

Dr. Mpango aagiza January, bosi Tanesco waende Kigoma Dr. Mpango aagiza January, bosi Tanesco waende Kigoma

MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango amewaagiza Waziri wa Nishati, January Makamba na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dk Tito Mwinuka waende Kigoma kushughulikia tatizo la kukatika umeme.

Dk Mpango alisema anataka hadi ikifika Oktoba 15 viongozi hao wampe taarifa kuhusu utekelezaji wa agizo hilo.

Alitoa agizo hilo Kasulu wakati akifungua maonesho ya biashara na viwanda yanayoratibiwa na Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO).

Dk Mpango aliagiza hayo baada ya Mbunge wa Kasulu Mjini, Profesa Joyce Ndalichako kumweleza kuwa maagizo aliyotoa kuhusu tatizo la kukatika umeme na kufikisha umeme kwa wananchihalijatekelezwa.

Profesa Ndalichako alisema bado kuna shida ya kupata umeme na wananchi wanahangaika kuungainishiwa nishati hiyo hivyo akaomuomba Dk Mpango atoe maelekezo kuhusu jambo hilo.

"Mheshimiwa Makamu wa Rais binafsi nimetembelea maeneo mbalimbali ya Wilaya Kasulu lakini nimeona mjini Kigoma bado umeme unakatika sana na pia upelekaji wa umeme kwenye maeneo ya wananchi kama ulivyoagiza haujafanyika vya kutosha, naomba upokee taarifa hii na utoe maelekezo yako," alisema.