Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 21Article 573277

Habari Kuu of Sunday, 21 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Ewura yawataka mafundi umeme kuwa na leseni

Ewura yawataka mafundi umeme kuwa na leseni Ewura yawataka mafundi umeme kuwa na leseni

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) imewataka wanafunzi wanaomaliza vyuo vya ufundi hasa waliobobea katika fani ya ufungaji wa mifumo ya umeme kuwa na leseni.

Hayo yamesemwa leo Jumapili Novemba 21, 2021 na Meneja wa Ewura Kanda ya Kaskazini, Mhandisi Lorivii Long'idu wakati alipotembelea chuo cha Karanga kilichopo Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.

"Tumekuja kwenye hiki chuo cha Karanga kwa ajili ya kuelimisha wanafunzi ambao tunajua ndio nguvu kazi inayokuja, katika kazi za ufungaji wa mifumo ya umeme inatakiwa ifanywe na mafundi ambao wana elimu,"amesema Long'idu

"Kwa hiyo tumekuja kutoa elimu hapa maana tunajua wanafunzi wakitoka hapa wanaenda mtaani kufanya kazi za ufungaji wa umeme na ili wafanye kazi hiyo wanatakiwa wawe na leseni kutoka Ewura,kwa mujibu wa sheria ya umeme"amesema

"Serikali ina mpango wa kupeleka umeme kwenye vijiji vyote nchini kwa hiyo tutakuwa na uhitaji mkubwa wa mafundi umeme wa kwenda kusaidia kufunga nyaya za umeme na kufanya "wiring" hivyo ni vyema wakawa na leseni kwa ajili ya shughuli hizi,"

"Uhitaji wa mafundi umeme nchini umekuwa mkubwa sana kwa sababu ya sera ya kupeleka umeme vijijini ambapo Serikali inataka kuhakikisha vijiji vyote vya nchi hii vitaitajika umeme" amesema Meneja huyo

Naye Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Luciana Tesha amewasihi wazazi kuwapeleka watoto wao katika chuo hicho ili waweze kujifunza mambo mbalimbali yanayohusiana na umeme ambayo yataweza kuwajenga katika kutafuta riziki za maisha.