Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 13Article 585493

Habari za Afya of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Fahamu Jinsi ya Kupika Vitumbua vya Nyama

Fahamu Jinsi ya Kupika Vitumbua vya Nyama Fahamu Jinsi ya Kupika Vitumbua vya Nyama

Hali yako mdau wa Nipe Dili kila jumanne leo kwa furaha na shangwe zote nataka kukufundisha kitu adimu kabisa na sio wote wanaotambua ufundi huu nakuletea mezani sasa.

Enhee huu ni msimu wetu wa kupeana madili ya jikoni tu kuhakiksha tunazisaka hata ikiwa shilingi mia 500 sikuruhusu hasa kuipotezea ungana na mimi kweneye nipe dili leo nikifundisha namna ya kupika vitumbua vya nyama unaionaje hiyo?

I hope itakua imekaa poa sana na nimejua kukusuprse wiki hii karibu tuingie mzigoni sasa kama ifutavyo zingatia maelekezo ili uweze kutoa kitu kizuri kijana mwenzangu.

Tuanze na Mahitaji mwanakwetu haya hapaa!

Nyama ya Kusaga robo

Kitunguu maji 1 tu

Kitunguu thoum nusu kijiko kile cha chakula

Karoti yako 1 inatosha hasa

Pilipili hoho mambo yanukie jaman 2tu

Mayai 5-6

Baking powder nusu kijiko kidogo

Pilipili mbichi( ukihitaji lakini)

Usisahau na chumvi pia

Haya sasa twenzetu jikoni tuangalie namna ya kupika vitumbua vya Nyama hatua kwa hatua.

Hakikisha umesafisha nyama yako vizuri itie vitunguu thoum, chumvi, pilipili manga na tangawizi, ibandike jikoni ili iive na ikauke vizuri.

Kisha kata kitunguu maji chako, hoho, pilipili, halfu vichanganye na mayai then vyote vitie kwenye nyama yako.

Weka kwenye Blenda mchanganyiko wetu usage kidogo lakini ili usiwe mlaini sana ukiwa tayari weka kwenye chombo ambacho unaweza kukaaa.

Baada ya hapo sasa weka baking powder, karoti na chumvi kidogo kisha changanya vizuri.

Enheee kisha andaa chuma cha kukaangia vitumbua bandika jikoni weka mafuta kidogo, mafuta yakipata moto chota rojo lako kwa upawa upo?

Utie kwenye kikaango vikiiva upande mmoja geuza na upande wa pili uive halafu uvitoe.