Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 24Article 553411

Diasporian News of Tuesday, 24 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Fedha za Uhamiaji kutumika Zanzibar

Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeweka utaratibu wa kutatua changamoto za muungano kupitia mfumo rasmi wa vikao vya kamati ya pamoja kati ya pande hizo mbili.

Haya yamebainishwa na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akiwa Zanzibar baada ya kumaliza ziara ya ukaguzi wa kiwanda cha maziwa cha fumba na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar.

“Fedha za Uhamiaji zinazotokana na shughuli za uhamiaji zinazopatikana Zanzibar zilikuwa zinahesabika kwenye bajeti za muungano na matumizi yake yalikuwa yanaidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini baada ya kuonekana hilo haliko sawa tulipitisha utaratibu kuwa sasa zitakusanywa Zanzibar na zinapangiwa matumizi Zanzibar".