Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 05Article 541138

Diasporian News of Saturday, 5 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Finland kuwapiga jeki maofisa maendeleo ya Jamii

Finland kuwapiga jeki maofisa maendeleo ya Jamii Finland kuwapiga jeki maofisa maendeleo ya Jamii

SERIKALI ya Finland imedhamiria kushirikiana na Tanzania kuhakikisha Maofisa Ustawi na Maendeleo ya Jamii wanawezeshwa katika utekelezaji wa shughuli zao za uboreshaji wa huduma kwa jamii hususani uwezeshwaji wanawake kiuchumi.

Hayo yalielezwa jana katika mazungumzo kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dk John Jingu na Mkuu wa Ushirikiano wa Ubalozi wa Finland nchini, Dk Timo Voipio yaliyofanyika jijini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo, Voipio alimhakikishia Katibu Mkuu Jingu kuwa Finland itaendelea kushirikiana na Tanzania kuhakikisha Maafisa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamii wanawezeshwa ipasavyo kuhakikisha huduma za Jamii zinaboreshwa.

Dk Timo ambaye pamoja na kubainisha mambo mbalimbali yanayofanywa na Serikali ya Finland nchini, alitaja kuwa uboreshaji wa utoaji wa huduma za kijamii ni moja ya vipaumbele vyao na watahakikisha wanashirikiana moja kwa moja na Serikali kuleta mabadiliko yanayoonekana.

Katibu Mkuu alisema wizara imeweka kipaumbele mkakati wa kuwawezesha maofisa hao vifaa vya kazi vikiwemo usafiri na vifaa vya kieletroniki ili kuwezesha ufanisi wa majukumu yao.

Kamishna wa Ustawi wa Jamii nchini, Dk Naftali Ng'ondi alisema serikali inatumia mbinu mbalimbali katika kuwezesha mikakati iliyowekwa ya kuwainua wanawake kiuchumi ikiwa ni pamoja na Sekta nyingine za maendeleo ya Jamii kuhusishwa katika utekelezaji wa mikakati hiyo.

Join our Newsletter