Uko hapa: NyumbaniHabari2021 12 07Article 576898

Habari Kuu of Tuesday, 7 December 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Forbes Yamtaja Rais Samia Kwenye Orodha ya Wanawake 100 Wenye Nguvu Zaidi Duniani

Forbes Yamtaja Rais Samia Kwenye Orodha ya Wanawake 100 Wenye Nguvu Zaidi Duniani Forbes Yamtaja Rais Samia Kwenye Orodha ya Wanawake 100 Wenye Nguvu Zaidi Duniani

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametajwa na Jarida maarufu duniani la takwimu na ripoti la Forbes katika orodha ya wanawake 100 wenye nguvu zaidi duniani kwa mwaka 2021.

Orodha hiyo inayojumuisha wanawake waliopo kwenye nyadhifa mbalimbali za juu duniani, wakiwemo marais, wafanyabiashara wakubwa na watu mashuhuri, imetangazwa leo, Desemba 7, 2021 na Jarida hilo kupitia tovuti yao ya www.forbes.com.

Rais Samia ambaye aliingia madarakani Machi 19, 2021 kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ametajwa kuwa katika nafasi ya 94 ya wanawake wenye nguvu zaidi ulimwenguni, huku uongozi wake imara na mapambano dhidi ya Corona, zikiwa ni sifa zilizompaisha zaidi.

Wengine waliotajwa katika orodha hiyo ni bilionea namba tatu duniani kwa upande wa wanawake, MacKenzie Scott ambaye ameshika namba moja akimwondoa Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel ambaye ameshika nafasi hiyo mara tatu ndani ya miaka 18.

Wa pili ni Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, Rais wa Benki Kuu ya Ulaya, Christine Lagarde ameshika namba tatu.

Wengine ni Rais wa Taiwan, Tsai Ing-wen, ambaye ameshika nafasi ya tisa, Gree Electric’s Dong Mingzhu (ameshuka chini nafasi 11 hadi nafasi ya 58) na Yum China CEO Joey Wat (ameshuka kwa nafasi 39 hadi nafasi ya  73).

Even Queen Elizabethnamba 70, Taylor Swift ameshika nafasi ya 78 na Ava Duvernay wa 80 na aliyekuwa mwajiriwa wa mtandano maarufu wa Facebook aliyedukua taarifa za mtandao huo na kuzianika kisha kuacha kazi, Frances Haugenamefunga ukurasa kwa kuwa namba 100.