Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 13Article 551350

Habari Kuu of Friday, 13 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

GEKUL: Pongezi kwa walioshiriki riadha Olimpiki

GEKUL: Tuwapongeze walioshiriki riadha Olimpiki GEKUL: Tuwapongeze walioshiriki riadha Olimpiki

Naibu waziri wa Ha bari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Pauline Gekul (Mb) amewataka watanzania kutopuuzia Jitihada zilizoonyeshwa na wachezaji wa Timu ya Taifa ya Riadha waliokwenda kushindana katika mashindano ya Olimpiki 2020 nchini Japan na kufanikiwa kuingia katika nafasi ya kumi (10) bora kwenye mbio ndefu za kilomita 42 Barabarani.

Mhe. Pauline ameyasema hayo tarehe 12 Agosti, 2021 wakati akiipongeza Timu iliyoshiriki katika mashindano ya Olimpiki na kuiaga Timu inayokwenda kushiriki mashindano ya Paralimpiki nchini Japan, katika hafla iliyofanyika katika hotel ya Blue Sapphire Jijini Dar es Salaam.

“Niombe watanzania wasipuuze jitihada zilizofanywa na wachezaji wetu wa riadha katika mashindano ya Olimpiki, bali tunatakiwa kuwapongeza kwa kulipambania Taifa katika mashindano hayo makubwa duniani licha ya kuwa na mabadiliko ya hali ya hewa lakini walipambana na tukamaliza katika nafasi ya kumi bora kwa mwanariadha wetu Alphonce Simbu kushika nafasi ya saba,tunatakiwa tujifunze kuthamini vya kwetu,”amesema Pauline.

Aidha Mhe. Pauline amesema wizara yenye dhamana ya michezo inayosimamiwa na Mheshimiwa Waziri Innocent Bashungwa imedhamiria kuendelea kuinua michezo nchini pamoja na kuipa nguvu michezo ya kipaumbele iendelee kufanya vizuri.

“Ndugu zangu naomba ifahamike kuwa wizara yetu imedhamiria kuendelea kuinua michezo nchini, lakini pia michezo ya kupaumbele tutaendelea kuipa nguvu iendelee kufanya vizuri,niseme tu kwamba viongozi wa vyama ambao hawawajibiki wajitathmini, Serikali yetu ya awamu ya Sita (6) inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ipo makini na haitawafumbia macho viongozi wa michezo ambao hawawajibiki,”amesema Mhe. Pauline.